Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeratibu usomaji wa Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani kwa watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s).
Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa, Shekhe Jawadi Nasrawi amesema “Maahadi imeandaa ratiba ya usomaji wa Qur’ani kwa watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika mwezi mtukufu wa Ramadhani”. Akasema kuwa “Ratiba hii inafanywa kwa mwaka wa nne mfululizo kwa lengo la kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani katika mwezi huu mtukufu”.
Akaongeza kuwa “Usomaji wa Qur’ani ni sehemu ya ratiba maalum iliyo andaliwa na Maahadi katika mwezi huu mtukufu, ratiba hiyo inahusisha usomaji wa Qur’ani, nadwa na vikao vya kielimu”.
Akaendelea kusema “Maahadi inaendeleza ratiba hiyo kwa kushirikiana na kikosi cha Abbasi (a.s), ikiwa ni pamoja na usomaji wa Qur’ani halafu thawabu za usomaji huo zinaelekezwa kwa mashahidi wa Iraq”.