Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kinafanya vikao vya kusoma Qur’ani kila siku kwa wanafunzi wa Dini wenye asili ya Afrika katika mji wa Najafu na Karbala, kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Vikao hivyo vinaratibiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo, kiongozi wa mradi wa Qur’ani katika Markazi Sayyid Dhwargham Ibrahimi amesema “Vikao vya usomaji wa Qur’ani vitadumu kwa muda wote wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa wanafunzi wa Dini wenye asili ya Afrika katika mji wa Najafu na Karbala”.
Akaongeza kuwa “Ratiba ya usomaji wa Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani ni mradi ambao hufanywa na Markazi kila mwaka, kwa lengo la kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii tofauti”, Atabatu Abbasiyya inajitahidi kunufaika na mazingira ya mwezi wa Ramadhani kwa kufundisha mambo mbalimbali yanayohusu Qur’ani na idaba.