Kitengo cha utumishi kinasafisha maeneo yote yanayozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, kinasafisha maeneo yote yanayozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kiongozi wa idara ya usafi chini ya kitengo Sayyid Muhammad Habibu Haadi amesema “Wahudumu wa kitengo cha utumishi, wanasafisha maeneo yote yanayozunguka jengo tukufu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya maeneo hayo kufurika idadi kubwa ya mazuwaru katika usiku wa Ijumaa”.

Akaongeza kuwa “Kazi hiyo inafanywa kwa lengo la kudumisha usafi na kuweka mazingira mazuri kwa mazuwaru watukufu” akasema kuwa “Wahudumu hufanya kila wawezalo katika kuhakikisha maeneo yote yanakuwa safi na yenye mpangilio mzuri, ili kutoa huduma bora kwa mazuwaru”.

Akasema kuwa “Wahudumu wa kitengo hiki wanafanya kazi kwa ustadi mkubwa kama zilivyo pangwa na idara, kwa lengo la kuhakikisha huduma bora kwa mazuwaru ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: