Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeratibu usomaji wa Qur’ani kwa kushirikiana na uongozi mkuu wa mazaru ya Zaidu Shahidi (a.s).
Kisomo hicho kinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil chini ya Majmaa, kuanzia saa kumi na moja jioni kila siku ndani ya mwezi wa Ramadhani.
Usomaji wa Qur’ani ni sehemu ya ratiba inayosimamiwa na Maahadi kwa ushiriki wa wasomaji wa kimataifa.
Nayo ni ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani iliyoandaliwa na Maahadi, kwa lengo la kuhuisha mwezi wa Ramadhani na kuweka mazingira bora kiimani, kundi kubwa la waumini linashiriki kwenye ratiba hiyo.