Matawi ya Maahadi ya Qur’ani upande wa wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu jijini Baghdad, wilaya ya Hindiyya, Munadharah yanatekeleza ratiba ya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kiongozi wa Maahadi bibi Manara Aljaburi amesema “Kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani, matawi na vituo vilivyo chini ya Maahadi vimeanza kutekeleza ratiba ya kusoma Qur’ani tukufu”.
Akaongeza kuwa “Ratiba ya vikao vya usomaji wa Qur’ani, inahusisha usomaji wa dua za mwezi wa Ramadhani, kufafanua maswala ya fiqhi na maarifa ya Qur’ani”, vikao hivyo vimepata muitikio mkubwa.