Idara ya maandalizi ya kongamano la vitabu kimataifa katika mji wa Qum, imezawadia kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kwa ushiriki mzuri kwenye kongamano hilo.
Kitengo kimeshiriki kipitia kituo cha upigaji wa picha nakala-kale na faharasi.
Kitengo kimeshiriki kutokana na mwaliko kiliopata kutoka katika uongozi wa Chuo kikuu cha Qum, ulio iomba Atabatu Abbasiyya ishiriki kwenye kongamano hilo.
Idara ya maandalizi ya kongamano imemkabidhi sheti cha ushiriki, mkuu wa kituo Sayyid Swalahu Siraji, kutokana na uwasilishaji mzuri wa mada yake kwenye kongamano hilo, aliyoipa jina la (Kutambulisha nafasi za maktaba na Daru-Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi kama mfano).
Pembeni ya kongamano hilo, umepongezwa ushiriki wa Atabatu Abbasiyya kupitia kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi kwenye kongamano la vitabu.