Sayyid Swafi ameanza kutoa mihadhara kuhusu dua ya Abu Hamza Shimali.

Mwalimu wa Hauza Allaamah Sayyid Ahmadi Swafi ameanza kutoa mihadhara ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu kuhusu dua ya Abu Hamza Shimali, mbele ya viongozi wa Dini, Hauza, baadhi ya viongozi wa Ataba na wahudumu wa Ataba.

Mwanzoni mwa maneno yake Sayyid Swafi ameanza kwa kupongeza wahudhuriaji kutokana na kuingia katika mwezi wa Ramadhani ambao Mwenyezi Mungu alishusha ndani yake Qur’ani na akajaalia katika mwezi huu kuna usiku bora kuliko miezi elfu, akamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu afunge milango ya moto na afungue milango ya pepo, huruma yake iwafikie waumini wote katika mwezi huu mtukufu.

Sayyid Swafi akasema kuwa, zaidi ya miaka minne iliyopita alitoa sherehe ya dua ya Abu Hamza Shimali, ambayo inatokana na Imamu Sajjaad (a.s), na leo anaendelea kukamilisha mfululizo huo mtukufu.

Tofauti ya mwezi huu, kwa mujibu wa ufafanuzi wa muheshimiwa, mwanaadamu hupunguza kula na kunywa na huongezeka uwezo wa akili na kutafakari, mwezi huu unamambo ambayo lazima yawe na athari kwa mwanaadamu, aidha ni kituo muhimu kwa kila mtu kutambua nafasi yake na mapungufu yake mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hivyo lazima tuutumie mwezi huu vizuri ili kila mtu aishinde nafsi yake.

Kuhusu dua, Muheshimiwa amesema kuwa, kuanzia mwanzo wa mwezi wa Ramadhani hadi mwisho Imamu (a.s) anatuonyesha kwa njia nzuri, tunatakiwa tuswali sana na kusoma dua sambamba na ibada zingine, akasema kuwa swala inanafasi kubwa mbele ya Imamu (a.s), kama ilivyo dua za Munajaat ni bora zaidi katika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, Maimamu (a.s) walikua wanajiliwaza kwa kusoma dua za Munajaat.

Akafafanua kuwa, mwanaadamu hupata amani na utulivu atakapokua mambo yake ya siri ni mema, hivyo lazima uifundishe nafsi yako kuwa njema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: