Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeanza kufanya maandalizi ya kushiriki kwenye maonyesho ya Qur’ani ya kimataifa awamu ya thelathini na moja jijini Tehran.
Rais wa Majmaa Dokta Mushtaqu Ali amesema, Majmaa-Ilimi ya Qur’ani tukufu itawakilisha Atabatu Abbasiyya kwenye maonyesho ya Qur’ani ya thelathini na moja jijini Tehran, imeanza kujiandaa kivitabu na kiutendaji.
Akaongeza kuwa “Ushiriki wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu kwenye maonyesho hayo unalenga kuonyesha shughuli zetu katika kuhudumia kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu”.