Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaendesha vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani katika mkoa wa Najafu.
Kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi ya Qur’ani tukufu mjini Najafu chini ya Majmaa, Sayyid Ahmadi Zaamili amesema “Maahadi inafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani tukufu ndani ya mwezi wa Ramadhani katika jengo la Baabul-Hawaaij Abulfadhil Abbasi (a.s) mkoani Najafu”.
Akaongeza kuwa “Kufuatia kuingia kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Maahadi inaendesha vikao vya usomaji wa Qur’ani kila siku katika mji wa Najafu kwa ushiriki wa wasomaji wakubwa watatu”.
Akaendelea kusema “Lengo la kufanya vikao vya kusoma Qur’ani ni kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii, sambamba na kufundisha usoamaji sahihi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu”.