Majmaa-Ilmi imeratibu hafla ya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wanaoishi bweni (hosteli) za chuo kikuu cha Karbala.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeratibu hafla ya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wanaoishi bweni (hosteli) za chuo kikuu za Karbala.

Kiongozi wa idara ya harakati za Qur’ani katika Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa Dokta Ali Hamdi amesema “Maahadi imeratibu hafla ya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wa bweni (hosteli) za chuo kikuu cha Karbala, kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa “Hafla hiyo inalenga kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani na kujenga hadhi ya wanafunzi wa chuo”, akasema “Inahusisha mashindano ya kusoma Qur’ani tukufu”.

Akaendelea kusema “Majmaa-Ilmi inafanya kila iwezalo katika kujenga uwelewa wa Qur’ani ambao ndio mwanga unaowaongoza katika njia sahihi wanafunzi wa chuo na kuwaweka katika mazingira mazuri chuoni na katika jamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: