Mwalimu wa hauza Allaamah Sayyid Ahmadi Swafi ametoa muhadhara wa kielimu wa pili katika mwezi wa Ramadhani, akisherehesha dua ya Abu Hamza Shimali mbele ya viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na wahudumu wake.
Muhadhara huo ni muendelezo wa mihadhara kama hiyo aliyotoa zaidi ya miaka minne iliyopita, katika ushereheshaji wa dua ya Abu Hamza Shimali kutoka kwa Imamu Sajjaad (a.s), katika mwezi huu mtukufu ameanza kusherehesha vipengele vya dua hiyo vinavyo husiana na mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Katika muhadhara wa pili amefafanua utukufu mwingi unaopatikana ndani ya mwezi huu, katika mwezi huu milango ya mbingu hufunguliwa, Mwenyezi Mungu hufunga milango ya moto na hufungua milango ya pepo, hadi vitendo vidogo usivyo vikusudia Mwenyezi Mungu hutoa thawabu, usingizi katika mwezi huu ni ibada, kupumua ni ibada, hiyo ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu.
Akabainisha kuwa, Hakika Mwenyezi Mungu ameweka Malaika maalum wanaoandika mema, wanahesabu pumzi za aliyefunga katika mwezi wa Ramadhani, akatoa wito wa kunufaika na mwezi huu mtukufu na kujiepusha ma maasi, utukufu wa mwezi huu unamfanya mwanaadamu ajione fakiri mbele ya Mwenyezi Mungu na ajitahidi kufanya vitendo vizuri na wala sio kufanya matendo mabaya lazima tuzinduke.
Akasema kuwa kusujudu ni njia bora zaidi ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, na mja huwa karibu zaidi na Mwenyezi Mungu anapokua sajda, kusujudi ni alama inayopambanua kati ya kiburi na kujidhalilisha.
Akafafanua kuwa lazima kujiandaa kinafsi katika kuamiliana na Mwenyezi Mungu mtukufu, kunyenyekea na kujielekeza kwake vimehimizwa na sheria takatifu.
Sayyid Swafi akahimiza kupambika na sunna za Mtume mtukufu na watu wa nyumbani kwake (a.s) kwa kufuata mwenendo wao, akasema kuwa kuswali mara nyingi na kusujudi ni jambo limehimizwa na sheria tukufu, wanachuoni wengi wanapopatwa na jambo linalowafadhaisha hukimbilia kwenye swala na hivyo ndio alivyokua Mtume (s.a.w.w), anapoingia kwenye swala anapata utulivu ambao hawezi kuupata mahala pengine, kunamazingatio kutoka kwa Imamu (a.s) ya kwamba alikua anapoingia katika swala anahisi yuko mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu.