Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kikao cha kujadili mahitaji ya vitengo vyake.

Idara ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kikao cha kujadili mahitaji ya vitengo vyake, na kuangalia kwa kina changamoto kubwa walizo nazo.

Kikao hicho kimeongozwa na makamo katibu mkuu wa Ataba Muhandisi Abbasi Mussawi Ahmadi.

Muheshimiwa Ahmadi amesema “Mkutano umefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), umehusisha wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya na marais wa vitengo na viongozi wao”.

Akaongeza kuwa “Kikao kimejadili njia za uboreshaji wa vitengo vya Ataba, sambamba na kujadili kwa kina mahitaji yao na muundo wake, tumejadili uboreshaji utakaoleta mafanikio kwa haraka, aidha tumetadili changamoto kuu na vikwazo vinavyo patikana katika baadhi ya kazi na kutafuta ufumbuzi ufaao”.

Kwa mujibu wa maelezo ya naibu katibu mkuu, kikao hicho kimetokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, kwa lengo la kupata mafanikio kwa njia sahihi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: