Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani kwa ushiriki wa wasomaji (250) katika mji mkuu wa Baghdad.
Usomaji huo wa Qur’ani unaratibiwa na Maahadi ya Qur’ani/ tawi la Baghdad chini ya Majmaa katika maeneo tofauti ya mji mkuu.
Kiongozi wa Maahadi Sayyid Nabiil Saidi amesema “Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinafanywa katika mji wa Karhka na Raswafah jijini Baghdad, pamoja na maeneo ya karibu na miji hiyo, washiriki wako zaidi ya wasomaji (250), kila siku wanasoma juzuu moja la Qur’ani tukufu ndani ya mwezi mzima wa Ramadhani.
Akaongeza kuwa “Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinapata muitikio mkubwa wa waumini usiku na mchana”.
Akasema kuwa “Maahadi ya Qur’ani tukufu huandaa ratiba maalum ya usomaji wa Qur’ani kila mwaka ndani ya mwezi wa Ramadhani, kwa lengo la kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa waumini”.