Chuo kikuu cha Al-Ameed kimesema: Kimefanikiwa kujikamilisha kielimu na kiidara.

Mkuu wa kitivo cha uuguzi katika chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Dhiyaa Karim amesema kuwa, kitivo kimejikamilisha kielimu na kiidara.

Mkuu wa kitivo cha uuguzi Dokta Dhiyaa Karim amesema “Chuo kikuu cha Al-Ameed na vitengo vyake vimejikamilisha kielimu na kiidara, nalo ni jambo la pekee katika vyuo vikuu vya Iraq, jambo hilo limesaidia kufikia malengo yake ya kutoa wataalamu bora”.

Akaongeza kuwa “Leo tunatoa pongezi kubwa kwa kitivo cha uuguzi kupata nafasi ya kwanza kwa ubora miongoni mwa vitivo vya uuguzi kutoka vyuo vikuu tofauti binafsi katika mwaka wa masomo 2023m, mafanikio hayo yametangazwa na shirika la (IRU) linalojihusisha na kufanya tathini za ubora wa kiidara na kielimu kwenye vyuo vikuu vya Iraq”.

Chuo kinatumia utaratibu wa kitaasisi katika kuendesha shughuli zake, ndio kilicho Saidia hadi kupata nafasi ya kwanza, kinamazingira mazuri ya kielimu na maabara bora yakisasa, kimejitahidi kutekeleza maono ya Atabatu Abbasiya tukufu katika kusimamia ubora.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: