Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya ratiba ya kidini kwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s) katika nchi ya Tanzania barani Afrika.
Ratiba hiyo imesimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo.
Mubalighi wa Markazi nchini Tanzania Shekhe Jamali Abdallah Kasole amesema “Markazi imefanya ratiba ya kidini kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika mji wa Dar es salaam nchini Tanzania katika siku hizi za mwezi mtukufu wa Ramadhani”.
Akaongeza kuwa “Ratiba imehusisha mihadhara ya kifiqhi, usomaji wa Qur’ani na baadhi ya ibada maalum katika mwezi huu mtukufu”.
Mubalighi wa Markazi amefundisha mada za Fiqhi, Aqida na Qur’ani kwenye hauza ya bibi Ummul-Banina (a.s) ya wasichana, katika mji wa Kigamboni uliopo jijini Dar es salaam nchini Tanzania.