Waziri wa utamaduni wa Iran Muhammad Mahadi Ismaili ametembelea tawi la Majmaa-Ilmi linaloshiriki kwenye maonyesho ya Qur’ani ya kimataifa awamu ya thelathini na moja jijini Tehran.
Rais wa Majmaa-Ilmi Dokta Mushtaqu Ali amemueleza Waziri mambo muhimu yatakayofanywa na tawi hilo katika siku za maonyesho.
Waziri ameonyesha furaha yake kwa ushiriki wa Atabatu Abbasiyya kwenye maonyesho hayo, amepongeza kazi zinazofanywa na Majmaa-Ilmi katika kutumikia kitabu cha Mwenyezi Mungu kielimu.
Majmaa-Ilmi inaonyesha mafanikio yake kwenye sekta ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya kupitia wahudumu wake wanaoshiriki kwenye maonyesho hayo, sambamba na kuonyesha picha halisi ya Ataba chini ya maelekezo ya Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria na uongozi mkuu wa Ataba.