Majmaa-Ilmi imefungua tawi lake kwenye maonyesho ya Qur’ani ya kimataifa jijini Tehran.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefungua tawi lake maalum katika maonyesho ya Qur’ani ya kimataifa awamu ya thelathini na moja jijini Tehran.

Shughuli za ufunguzi wa tawi hilo zimehudhuriwa na rais wa Majmaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya Dokta Mushtaqu Ali pamoja na viongozi wengine.

Muheshimiwa Ali ameshukuru mualiko uliotolewa kwa Atabatu Abbasiyya wa kuja kushiriki kwenye maonyesho hayo, akasema kuwa uwepo wa Ataba tukufu katika maonyesho hayo kunaongeza mazingira ya kiroho kwa wadau wa maonyesho.

Rais wa Majmaa-Ilmi amepokea viongozi waliotembelea tawi la Atabatu Abbasiyya na kufafanua mambo muhimu yanayofanywa na tawi hilo, ambapo ni kuonyesha vitabu, kuendesha mashindano na mambo mengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: