Atabatu Abbasiyya inaomboleza kifo cha bibi Khadijatu-Kubra (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu imeomboleza kifo cha bibi Khadijatu-Kubra (a.s) na kumpa pole Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa kufiwa na mkewe aliyetoa mchango mkubwa katika kunusuru Dini ya Uislamu.

Maombolezo yamepambwa na vipengele tofauti, uwekaji wa mapambo yanayo ashiria huzuni na utoaji wa mihadhara ya kuomboleza.

Mihadhara imejikita katika kueleza historia ya bibi Khadija na msaada wake kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), sambamba na kueleza mchango wake katika kunusuru Uislamu na namna alivyo jitolea katika kutangaza haki.

Katika kuomboleza msiba huo, wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wamefanya kisimamo na kutoa pole kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu hutoa kipaombele zaidi katika kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa ajili ya kuwatambulisha na kuwakumbuka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: