Sayyid Swafi ametoa muhadhara ya tano katika kusherehesha dua ya Abu Hamza Thamali.

Mwalimu wa hauza Allaamah Sayyid Ahmadi Swafi ametoa muhadhara wa tano katika kusherehesha dua ya Abu Hamza Thamali mbele ya viongozi na wahudumu wa Ataba tukufu.

Muhadhara wa tano ni sehemu ya muendelezo wa mihadhara aliyokuwa akitoa zaidi ya miaka minne iliyopita, katika kusherehesha dua ya Abu Hamza Thamali kutoka kwa Imamu Sajjaad (a.s), katika mwezi huu mtukufu anafafanua vipengele vinavyohusiana na mwezi wa Ramadhani.

Sayyid Swafi atanabahisha aliyokwisha eleza kuhusu kughafilika na athari zake, huwa ni sababu ya kukosa baraka nyingi na madhumuni ya dua ya Imamu (a.s) amefungamanisha na kukata tamaa katika rehema za Mwenyezi Mungu mtukufu.

Amesisitiza kushikamana na haki na kufuata mwenendo sahihi, pamoja na mambo mazuri kwa mwanaadamu huongeza utiifu kwa Mwenyezi Mungu na kumuepusha na kughafirika, dua ya Imamu inavipengele vinavyo onyesha athari za vitendo vibaya na mambo yanayofungamana navyo.

Akasema kuwa, matendo maovu mtu huona ladha kwa muda mfupi ni sawa na mawingu yapitayo, kwa mfano mtu anayefanya jambo la haram atalifurahia kwa muda mfupi kisha litaisha, siku ya kiyama atakapoona madhambi yake atajuta kwanini alifanya.

Akabainisha kuwa mwanaadamu anapupa, hatambui jambo lenye faida nae, atakapokuja kuona uhakika wa mambo siku ya kiyama atasema (Nirudisheni ili niweze kufanya mema), lakini hatokubaliwa muda umeshaisha, mtu anapopatwa na matatizo hurejea kwa Mwenyezi Mungu na kujinyenyekeza kwake, matatizo yanapoisha husahau na kurudi katika maovu kama alivyokua awali, anadhani anamdanganya Mwenyezi Mungu mtukufu, kumbe anajidanganya mwenyewe.

Muheshimiwa akaongea kipengele kilichopo kwenye dua ya Imamu (a.s) kuhusu vikao vya haram visivyo mridhisha Mwenyezi Mungu mtukufu, na athari ya kukaa kwenye vikao vya haram na kuchanganyika na watu wanaofanya batili, jambo hilo ni mtihani kwa mwanaadamu.

Akabainisha baadhi ya uwelewa kuhusu namna Mwenyezi Mungu anavyo kubali maombi, na tofauti ya dua ya muumini na mnafiki, akaeleza namna riwaya zinavyo himiza kumuomba Mwenyezi Mungu wakati wa raha na shida, Mwenyezi Mungu anapenda kusikia maombi ya mwanaadamu wakati wote, hakika hilo ni jambo tukufu sana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: