Tawi la Atabatu Abbasiyya linaloshiriki kwenye maonyesho ya Qur’ani jijini Tehran limefanya kikao cha usomaji wa dua ya Kumail.
Tawi la Ataba chini ya usimamizi wa Majmaa-Ilmi linavipengele tofauti kwenye maonyesho ya kimataifa ya awamu ya thelathini na moja.
Msomaji wa Atabatu Abbasiyya Muhammad Ridhwa Zubaidi amesoma dua mbele ya wadau wengi wa maonyesho katika mazingira ya kiroho yaliyo fasiriwa na machozi ya wahudhuriaji.
Majmaa-Ilmi inajitahidi kuonyesha matukio yanayohusu Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya mbele ya washiriki wa maonyesho na kuonyesha picha halisi ya Ataba tukufu kwa mujibu wa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria na uongozi wa juu.