Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya opresheni kubwa ya kusafisha maeneo yote yanayozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kiongozi wa idara ya usafi Sayyid Muhammad Habibu Haadi amesema “Wahudumu wa kitengo chetu wamefanya usafi mkubwa asubuhi ya Ijumaa, wamesafisha maeneo yote yanayozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya maeneo hayo kufurika watu wengi siku ya Alkhamisi ya jana”.
Akaongeza kuwa “Miongoni mwa kazi walizofanya ni kusafisha mlango wa Qibla, mzunguko wa Ataba tukufu, uwanja wa Alqami, sehemu za nje zenye paa na kutupa taka zote zilizokuwepo kwenye pipa za taka”.
Akabainisha kuwa “Wahudumu wetu hufanya kila wawezalo kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu, na hujitahidi kuongeza huduma zaidi katika siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani”.