Kitengo cha Habari na utamaduni kinaendelea na ratiba ya mwanafunzi hodari katika mkoa wa Dhiqaar.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kinaendelea na ratiba ya (mwanafunzi hodari) katika mkoa wa Dhiqaar.

Ratiba hiyo inasimamiwa na kituo cha kitamaduni Multaqal-Qamaru chini ya kitengo.

Ratiba imelenga wanafunzi wa shule za sekondari (upili) na shule za ufundi katika mji wa Naswiriyya hapa mkoani, kwa lengo la kujenga uwezo wa kielimu na maarifa kwa kundi hilo muhimu katika jamii.

Ratiba imepambwa na mihadhara mingi ya kielimu na kitamaduni pamoja na harakati tofauti.

Ratiba ya (mwanafunzi hodari) ni miongoni mwa harakati muhimu zinazofanywa na kituo kwenye shule na vyuo tofauti kwa lengo la kujenga uwezo wa vijana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: