Idara ya Fatuma binti Asadi inaendesha vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Idara ya Fatuma binti Asadi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendesha vikao vya usomaji wa Qur’ani kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani chini ya ushiriki wa idara za wasichana.

Kiongozi wa idara bibi Fatuma Mussawi amesema “Idara inaendesha vikao vya usomaji wa Qur’ani katika kituo cha Swidiqatul-Kubra (a.s), chuo kikuu cha Al-Ameed, Nyumba za makazi za Abbasi (a.s) kwa zaidi ya vikao kumi kwenye kila eneo”.

Akaongeza kuwa “Vikao vinafanywa kwa ushiriki wa Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya idara ya wasichana, idara ya shule za Alkafeel za wasichana na vinapambwa na ufundishaji wa kusoma Qur’ani tukufu, mashindano ya Qur’ani pamoja na kuadhimisha matukio ya Ahlulbait (a.s) yaliyotokea ndani ya mwezi huu mtukufu”.

Akaendelea kusema “Idara imefanya aina fulani ya matembezi katika utekelezaji wa ratiba hiyo, imewaalika washiriki wa ratiba hiyo katika kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) kwa ajili ya futari”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: