Mjumbe wa Majlisi shura ya Qur’ani tukufu nchini Iran Sayyid Abbasi Anjaami, amepongeza ushiriki wa Atabatu Abbasiyya katika maonyesho ya Qur’ani ya kimataifa yanayofanyika jijini Tehran.
Ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea tawi la Ataba tukufu na kuangalia shughuli zinazofanywa na tawi hilo pamoja na ratiba zingine tofauti.
Akasema kuwa “Harakazi za Qur’ani zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya zinamaendeleo makubwa, zinamchango mkubwa katika kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani dunia nzima”, akaonyesha namna alivyo furahishwa na mambo aliyoshuhudia katika tawi la Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu na mafanikio yake.
Majmaa-Ilmi inaonyesha mafanikio ya Atabatu Abbasiyya kwenye sekta ya Qur’ani kwa washiriki wa maonyesho hayo, pamoja na kuonyesha picha halisi ya Ataba chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria na uongozi mkuu.