Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu inaendesha ratiba yenye anuani isemayo “Andika barua kwa Imamu wa Zama” katika tawi la Atabatu Abbasiyya kwenye maonyesho ya Qur’ani ya kimataifa yanayoendelea jijini Tehran.
Mtu anaandika barua na kuikabidhi kwenye tawi la Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu, kwenye barua hiyo anaandika hisia zake na dua yake kuhusu Imamu wa Zama (a.f) halafu anaweka kwenye sanduku maalum, barua zitakusanywa na kuwekwa juu ya dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s).
Ratiba imepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru, wameonyesha kufurahishwa nayo na mapenzi ya Kwenda kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s) na hamu kubwa ya Imamu wa Zama (a.f).