Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya nadwa ya wazi katika mkoa wa Dhiqaar.
Nadwa hiyo ni sehemu ya ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani inayotekelezwa na kituo cha kitamaduni Multaqal-Qamaru.
Nadwa imepata mahudhurio makubwa ya vijana na walimu kutoka maoneo tofauti ya mkoa, ambapo mambo mbalimbali yamejadiliwa.
Ratiba ya mwezi wa Ramadhani ni moja ya ratiba maalum ambayo hufanywa na kituo ndani ya mwezi huu mtukufu, kwa lengo la kunufaika kielimu na kiimani watu wa tabaka tofauti katika jamii.