Sayyid Swafi anatoa muhadhara wa sita katika mwezi wa Ramadhani anasherehesha dua ya Abu Hamza Thamali.

Mwalimu wa hauza Allaamah Sayyid Ahmadi Swafi ametoa muhadhara wa sita katika mwezi wa Ramadhani, akisherehesha dua ya Abu Hamza Thamali mbele ya viongozi na wahudumu wa Ataba.

Muhadhara huo ni sehemu ya mfululizo wa mihadhara aliyotoa zaidi ya miaka minne iliyopita ya kusherehesha Dua ya Abu Hamza Thamali ya Imamu Sajjaad (a.s), mwezi huu mtukufu ameanza kusherehesha vipengele vinavyo husiana na mwezi wa Ramadhani.

Sayyid Swafi ameanza kwa kukumbusha muhadhara uliopita, kuhusu mambo ambayo huondoa mafanikio kwa mwanaadamu, na madhambi yenye athari duniani na akhera, akataja mambo yaliyosemwa na Imamu (a.s) kuhusu kumkanusha Mwenyezi Mungu na kupuuza haki zake, kukaa kwenye vikao viovu, kutokaa kwenye vikao vya wanachuoni, kutoshukuru, kughafirika na athari zake kwa mwanaadamu.

Akaeleza ulazima wa kumtegemea Mwenyezi Mungu mtukufu na kuhisi kumuhitaji kama vile fakiri anavyomuhitaji Tajiri, kwasababu uhusiano wa mja na Mwenyezi Mungu ni sawa na uhusiano wa mtu fakiri na bosi Tajiri, uhitaji huo unaonyesha namna ya kumuelekea Mwenyezi Mungu mtukufu, pia unamfanya mwanaadamu kuwa na tahadhari katika matendo yake, anatakiwa ajue kuwa akifanya baya atalibwa duniani au akhera, mambo hayo yatamsaidia kuwa na khofu na kufuata mwenendo sahihi.

Kuhusu riziki na Imani akasema, kuamini kuwa Mwenyezi Mungu mtukufu ndio mtoaji wa riziki mwenye hekima, hukadiria maslahi ya mwanaadamu katika utajiri na ufakiri, kwani yeye ni mjuzi zaidi, jambo hilo husaidia kuwa na utulivu wa nafsi kwa mwanaadamu, Mwenyezi Mungu mtukufu anaona mambo yaliyofichikana, mambo yote yanarejea kwake, anaweza kubadilisha jambo lolote, itikadi hiyo humfanya mwanaadamu akapata utulivu.

Akasema kuwa kutonufaika na Mwenyezi Mungu ni hasara.

Akafafanua vipengele katika dua ya Abu Hamza na kuonyesha mfungamano wake katika kutafuta rehema za Mwenyezi Mungu mtukufu, yote katika mlango wa rehema za Mwenyezi Mungu mtukufu katika kuelezea baadhi ya Adabu za dua.

Akafafanua kuwa miongoni mwa Adabu za dua kwa mwanaadamu, ni kuuzowesha ulimi wake kumtaja Mwenyezi Mungu au baadhi ya sifa zake wakati wote, katika dua ya Iftitaahi na zinginezo kuna maneno yanayo onyesha upole wa Mwenyezi Mungu mtukufu.

Muhadhara wa Sayyid Swafi umehimiza kumkimbia shetani, kujiepusha kufungamana zaidi na dunia, kurejea katika rehema za Mwenyezi Mungu na upole wake, akaeleza kuwa mtu anapomdhania Mwenyezi Mungu vizuri ni matokeo ya kwamba Mwenyezi Mungu atamfanya kuwa mwema, dhana nzuri hufungamana na ukarimu na upole, na Mwenyezi Mungu ni mkarimu anamambo yote mazuri hawezi kumuangusha mja wake aliyemdhania vizuri kisha asimpe yale mazuri yaliyotarajiwa kwake na mja wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: