Wasomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameshiriki kwenye hafla za matawi yanayoshiriki kwenye maonyesho ya kimataifa jijini Tehran.

Wasomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameshiriki katika usomaji wa Qur’ani unaofanywa na matawi yanayoshiriki kwenye maonyesho ya Qur’ani ya kimataifa jijini Tehran awamu ya Thelathini na moja.

Vikao walivyoshiriki wasomaji wa Ataba vimepata muitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa maonyesho, watu wengi wanahamu ya kuwaona wawakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwani wanazawadi kutoka kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Matawi yanayoshiriki kwenye maonyesho hayo ya kimataifa, yanaendelea kuwaalika wasomaji wa Atabatu Abbasiyya kwenye vikao vya usomaji wa Qur’ani vinavyo fanywa pembezoni ya maonyesho hayo, kama sehemu ya kuongezeka kwa ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kunufaika na mwanga wa malalo ya Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: