Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimehuisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hassan (a.s) katika viwanja vya ukanda wa kijani.

Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya nchini Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu, chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimeadhimisha mazazi ya Imamu Hassan (a.s) katika viwanja vya ukanda wa kijani.

Sayyid Ali Karim mmoja wa wasimamizi wa ratiba hiyo amesema “Kitengo kimefanya hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hassan (a.s) katika viwanja vya ukanda wa kijani”.

Akaongeza kuwa “Hafla imepambwa na tenzi na mashairi kuhusu Imamu Hassan (a.s) yaliyoimbwa kwa mahadhi mazuri mbele ya familia za wakazi wa Karbala”.

Atabatu Abbasiyya tukufu na vitengo vyake huzingatia sana kuhuisha matukio ya kuzaliwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kwa lengo la kuelezea historia zao na kufuata mwenendo wao mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: