Kiongozi wa jumba la uandishi wa Msahafu nchini Iran ametembelea tawi la Atabatu Abbasiyya.

Kiongozi wa jumba la uandishi wa Msahafu nchini Iran, Sayyid Mahadi Babaaiy ametembelea tawi la Atabatu Abbasiyya linaloshiriki kwenye maonyesho ya Qur’ani ya kimataifa jijini Tehran.

Tawi la Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya limeandaa ratiba maalum yenye vipengele vya usomaji wa Qur’ani, shughuli za kitamaduni na mashindano kwa mazuwaru, sambamba na ugawaji wa zawadi za tabaruku na watu kupewa fursha ya kubusu bendera iliyokuwa juu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu Dokta Mushtaqu Ali amekutana na Sayyid Mahadi Babaaiy, akamueleza kuhusu shughuli zinazofanywa na tawi la Ataba ikiwemo uandishi wa nakala maalum ya msahafu wa Atabatu Abbasiyya, ambapo alionyesha kufurahishwa na nakala hiyo pamoja na machapisho mengine.

Babaaiy akasema kuwa Jumba la uandishi wa msahafu chini ya kituo cha uchapishaji na usambazaji wa Qur’ani tukufu katika taifa la Iran, wanajivunia kuwa na ushirikiano na Atabatu Abbasiyya katika sekta ya uchapishaji wa misahafu na shughuli zingine zinazohusu Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: