Wizara ya utamaduni ya Iran imepongeza ushiriki wa Atabatu Abbasiyya kwenye maonyesho ya kimataifa jijini Tehran.

Rais wa taasisi ya utamaduni na uhusiano chini ya wizara ya utamaduni ya Iran Dokta Muhammad Mahadi Imani Buri amepongeza ushiriki wa Atabatu Abbasiyya kwenye maonyesho ya Qur’ani ya kimataifa jijini Tehran.

Ametoa pongezi hizo alipotembelea tawi la Atabatu Abbasiyya linalosimamiwa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu na kuona mambo mbalimbali yanayofanywa na tawi hilo.

Imani Buri ametabaruku kwa bendera ya malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), akaonyesha furaha yake kwa kutembelea tawi hilo, akasema kuwa uwepo wa tawi hilo kwenye maonyesho haya kunawakilisha nuru ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa taasisi ya utamaduni na mahusiano chini ya wizara ya utamaduni ya Iran amepongeza vitu alivyoshuhudia kwenye tawi la Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu na mafanikio yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: