Idara ya Fatuma binti Asadi inaendesha shindano la Qur’ani liitwalo (Aayaatun-Lisaailiina)

Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imetangaza kuendesha mashindano ya Qur’ani kwa jina la (Aayaatun-Lisaailiina), katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Masharti ya shindano ni:

  • 1- Shindano la wanawake tu.
  • 2- Majibu yatokane na kitabu cha (Masomo ya awali katika tafsiri ya Ayaatul-Ahkaam).
  • 3- Uandike jibu kwenye karatasi na kukabidhi moja ya sehemu zifuatazo: (Karbala tukufu – mtaa wa Mulhaq – Markazi Swidiqatu Twahirah – Ghorofa la tatu.
  • 4- Majibu hayatapokelewa baada ya kutangazwa matokeo.

Mwisho wa kupokea majibu ni tarehe (7/4/2024m sawa na 27 Ramadhani tukufu).

Washindi watatu wa mwanzo watapewa zawadi kama ifuatavyo:

  • 1- Mshindi wa kwanza 100,000 Dinari za Iraq.
  • 2- Mshindi wa pili 75000 Dinari za Iraq.
  • 3- Mshindi wa tatu 50,000 Dinari za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: