Kitengo cha Dini kimeadhimisha mazazi ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeadhimisha mazazi ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kupitia mihadhara mbalimbali ya kidini.

Rais wa kitengo Shekhe Swalahu Karbalai amesema: “Kitengo kimeadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa kutoa mihadhara ya kidini kabla ya swala ya Dhuhurain ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Mihadhara imejikita katika kueleza Maisha ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kuanzia kuzaliwa kwake, wakati wa uhai wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), wakati wa Imamu Ali (a.s) na wakati wa uongozi wake (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya tukufu huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa kufanya mambo mbalimbali, ikiwemo utoaji wa mihadhara elekezi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: