Kongamano la Nuru mbili awamu ya tatu limeshuhudia shindano la (kijana mbunifu) miongoni mwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Kongamano linasimamiwa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kupitia Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Baabil kwa kushirikiana na uongozi maalum wa mazaru ya Zaidu Shahiid (a.s).
Mkuu wa Maahadi Sayyid Muntadhiru Mashaikhi amesema “Shindano la (Kijana mbunifu), limeratibiwa kupitia shughuli za kongamano la Nuru mbili awamu ya tatu, limelenga wanafunzi wa shule za msingi na sekondari”.
Akaongeza kuwa “Shindano lilikuwa na sehemu mbili: Sehemu ya kwanza kuhifadhi usia wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa waumini wote, sehemu ya pili usomaji wa mashairi kwa lugha ya kiarabu fasaha”.
Shindano la (Kijana mbunifu), linalenga kuibua vipaji vya wanafunzi na kuviendeleza, sambamba na kuwatambulisha Ahlulbait (a.s) katika nyoyo za wanafunzi, kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa Maahadi.