Majmaa-Ilmi imeadhimisha mazazi ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika mkoa wa Dhiqaar.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeadhimisha mazazi ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa kufanya kikao cha usomaji wa Qur’ani katika mkoa wa Dhiqaar.

Kikao hicho kimesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Dhiqaar chini ya Majmaa.

Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinafanywa chini ya ratiba iitwayo (Amana tuliyopewa), ya kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s) chini ya usimamizi wa Maahadi.

Ratiba imepambwa na mahafidhu wa Qur’ani tukufu pamoja na mahafidhu wa Nahaju-Balagha, imehudhuriwa na kundi kubwa la waumini kutoka sehemu tofauti za mkoa, washindi wa mashindano tofauti wakapewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: