Atabatu Abbasiyya imewekwa mapambo meusi na mabango yanayo ashiria huzuni.

Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wameweka mabango yanayoashiria huzuni katika kujiandaa na kuomboleza kifo cha Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).

Makamo rais wa kitengo hicho Shekhe Zainul-Aabidina Quraish amesema “Wahudumu wa kitengo chetu wameweka mapambo yanayoashiria huzuni kwenye maeneo ya Ataba tukufu, kama sehemu ya maandalizi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Mabango yamewekwa katika eneo la ukumbi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yanayozunguka sehemu hiyo, wanaendelea kuweka sehemu zingine, wanatumia vifaa maalum katika uwekaji wa mabango hayo”.

Akaendelea kusema “Wahudumu wetu wamesambaza zaidi ya nakala elfu 20 za Qur’ani tukufu ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wameandaa sehemu maalum kwa ajili ya kufanya ibada za Lailatul-Qadri, sambamba na kuweka vitabu vingi vya dua”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: