Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).
Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala, imehudhuriwa na watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kundi la mazuwaru.
Mhadhiri wa Majlisi Shekhe Naim Saidi amesema “Tumetoa muhadhara ndani ya ukumbi wa utawala katika Ataba kuhusu sifa za uongozi, tumeangazia sifa za kiongozi kutoka kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) na athari yake katika umma, tukaeleza kuhusu ushujaa pia”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya inafanya kazi kubwa inayostahiki pongezi, hususan kwenye sekta ya Elimu, Tablighi na utoaji wa huduma za kijamii”.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s), sambamba na kuandaa mazingira bora na tulivu kiibaba.