Mawakibu za mji wa Karbala zinaomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s) mbele za malalo ya watoto wake.

Mawakibu za watu wa Karbala, zimeomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mawakibu zilianza kuomboleza zaidi ya siku mbili zilizopita na zitaendelea baada ya tarehe ya kifo chake, wanaanza kuomboleza jioni na wanaendelea hadi wakati wa swala ya Alfajiri, asilimia kubwa ya mawakibu zinazoshiriki ni za wakazi wa Karbala na maeneo ya jiraji na mji huo.

Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimeandaa ratiba maalum ya matembezi ya mawakibu hizo.

Mmoja wa viongozi wa mawakibu Sayyid Abu Swalehe Ali amesema “Watu wa Karbala wamezowea kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s) katika nyakati hizi”.

Akaongeza kuwa “Kama kawaida, mawakibu huanza matembezi yake katika Barabara zinazoelekea kwenye haram za malalo mbili takatifu huku wakiimba qaswida na tenzi za kuomboleza ambazo huamsha hisia ya huzuni katika nyoyo za waumini”.

Uombolezaji haukufanywa na mawakibu peke yake, bali mazuwaru wameshiriki kikamilifu katika kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: