Atabatu Abbasiyya tukufu kwa siku ya pili mfululizo, inaendelea na majlisi za kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s).
Majlisi zinasimamiwa na idara ya wahadhiri katika Ataba tukufu.
Majlisi imehudhuriwa na wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru, ndani ya ukumbi wa utawala katika Ataba tukufu, itaendelea kwa muda wa siku nne.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na muhadhara kuhusu kifo cha kiongozi wa waumini (a.s), halafu ikafuata mihadhara ya mambo tofauti kuhusu Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).
Muhadhiri ameeleza kuhusu Maisha ya Imamu Ali (a.s), ushujaa wake, ufasaha wake, kujitolea kwake, jinsi alivyolinda uislamu na mazingira ya kifo chake, kisha akahimiza kufuata mwenendo wake.
Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum yenye vipengele tofauti katika kuomboleza msiba huu.