Makundi ya mazuwaru yameomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) na Lailatul-Qadri ya pili katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Ataba tukufu umeshuhudia makundi makubwa ya waombolezaji waliokuja kufanya ziara na kusoma dua ya usiku wa (21) katika mwezi wa Ramadhani (Lailatul-Qadri ya pili) na kuomboleza kifo cha Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).
Mazuwaru huadhimisha siku hii tukufu kwa kusoma dua maalum, kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kuinua misahafu na kufanya vikao (Majlisi) za kuomboleza.
Atabatu Abbasiyya imeandaa vitu vyote vinavyo hitajika katika kufanya ibada, mazuwaru huanza kufanya ibada za Lailatul-Qadri baada ya Isha na huendelea hadi asubuhi, katika mazingira tulivu yaliyojaa huzuni ya kufiwa na kiongozi wa waumini (a.s).