Majmaa-Ilmi inahuisha usiku wa Lailatul-Qadri katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f).

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imehuisha usiku wa Lailatul-Qadri katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f).

Kiongozi wa idara ya tahfiidh katika Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa Shekhe Ali Rawii amesema “Maahadi kwa kushirikiana na kitengo cha Maqaam imehuisha usiku wa Lailatul-Qaqri kwa ushiriki wa wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani na walimu wao”.

Akaongeza kuwa “Harakati hii ni sehemu ya ratiba ya Maahadi ya Qur’ani katika kuhuisha siku tukufu za Lailatul-Qadri”.

Akabainisha kuwa “Vikao vya usomaji wa Qur’ani na kuhuisha siku za Lailatul-Qadri kuna umuhimu mkubwa, kutokana na hadithi ya Mtume (s.a.w.w) inayo tutaka kushikamana na vizito viwili ambavyo ni kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume (s.a.w.w)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: