Wizara ya elimu ya juu imekizawadia chuo kikuu cha Al-Ameed kwa kuwa na mfumo bora wa kichuo.

Wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, imekizawadia chuo kikuu cha Al-Ameed kwa kupata nafasi ya kwanza ya ubora wa vyuo vikuu vya Iraq.

Zawadi imetolewa katika kikao cha Waziri wa elimu ya juu Dokta Naim Al-Abudi na rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Judat Nuri.

Al-Abudi amepongeza chuo kwa kupata nafasi ya kwanza katika ubora wa vyuo vikuu vya Iraq, akahimiza ulazima wa kuendelea kuboresha huduma za kielimu na kitafiti, ili kuonyesha uwepo wa Iraq kimataifa na kuendelea kutoa upinzani katika uga wa elimu kimataifa.

Mwisho wa kikao chao Dokta Naim Al-Abudi akakabidhi zawadi ya chuo kikuu cha Al-Ameed kwa kupata tuzo ya ubora katika vyuo vikuu vya Iraq mwaka 2023m na kujipambanua kitaasisi na kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: