Watu wa Karbala wanaomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s) katika mji wa Najafu.

Watu wa mji wa Karbala wameomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s) kupitia maukibu ya pamoja mbele ya malalo yake takatifu katika mji wa Najafu.

Rais wa kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Aqiil Yaasiri amesema “Watu wa Karbala kila mwaka hufanya maukibu ya pamoja katika kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) mbele ya malalo yake takatifu katika mji wa Najafu”.

Akaongeza kuwa “Maukibu imefanya matembezi ya kuomboleza yaliyoanzia katika moja ya Barabara zinazoelekea kwenye haram ya Alawiyya, maukibu hiyo imejumuisha makundi na Husseiniyya tofauti za watu wa Karbala, mwisho wa matembezi hayo ilikuwa ndani ya haram tukufu ya Imamu Ali (a.s) ambapo wamefanya Majlisi ya kuomboleza.

Akaendelea kusema “Ataba mbili tukufu zinamchango mkubwa katika kuandaa na kusimamia maukibu hiyo, ikiwa ni pamoja na kuandaa gari maalum kwa ajili ya kubeba mazuwaru, kuwapeleka Najafu na kuwarudisha Karbala, uratibu wa shughuli za maukibu chini ya usimamizi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: