Atabatu Abbasiyya imeandaa msafara wa gari 400 kupeleka mazuwaru katika mji wa Samaraa kufanya ibada za usiku wa Lailatul-Qadri.

Atabatu Abbasiyya imeandaa msafara wa gari 400 kupeleka mazuwaru kufanya ibada za Lailatul-Qadri ya tatu mbele ya malalo ya Maimamu wawili Askariyaini (a.s) katika mji wa Samaraa.

Rais wa ugeni wa Ataba tukufu Sayyid Khaliil Hanuun amesema “Chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, Atabatu Abbasiyya imezowea kupeleka mamia ya mazuwaru kutoka Karbala na mikoa mingine kwenda kufanya ibada za Lailatul-Qadri mbele ya malalo ya Maimamu wawili Askariyaini (a.s) katika mji wa Samaraa”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imeandaa gari 400 zenye ukubwa tofauti kwa ajili ya kubeba mazuwaru chini ya makubaliano na Atabatu Askariyya tukufu, ambayo imefanya kila iwezalo katika kurahisisha ziara na ibada maalum za Lailatul-Qadri”.

Akabainisha kuwa “Ratiba ya ziara inahusisha usomaji wa Qur’ani tukufu na ugawaji wa futari, kisha mazuwaru huanza kufanya ibada maalum za usiku wa Lailatul-Qadri ambao ni bora kushinda miezi elfu moja ndani ya haram takatifu ya Maimamu wawili Askariyaini (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: