Kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) katika Atabatu Abbasiyya kimehuisha siku za Lailatul-Qadri kwa ushiriki wa makundi ya mazuwaru.
Kiongozi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba tukufu bibi Taghridi Tamimi amesema “Makundi ya mazuwaru yalijaa katika eneo malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kufanya ibada maalum la Lailatul-Qadri, Majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s) na kufanya igizo lenye anuani isemayo (Uvamizi habari kubwa), limefanywa na idara ya wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba tukufu”.
Akaongeza kuwa “Ibada hufunguliwa kwa kusoma sura maalum na kutoa maelekezo ya usomaji wa dua kama ilivyopokewa kutoka kwa Ahlulbait (a.s) katika usiku wa ishirini na tatu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, bila kusahau dua ya kuinua misahafu”.
Akaendelea kusema “Ibada hukamilishwa kwa kusoma dua ya Faraj ya Imamu Mahadi (a.s)”.