Idara ya Dini imekamilisha ratiba maalum ya kuhuisha siku za Lailatul-Qadri.

Idara ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha ratiba maalum ya kuhuisha siku za Lailatul-Qadri katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kiongozi wa idara hiyo, bibi Adhraa Shami amesema “Sardabu ya Imamu Hussein (a.s) katika Ataba tukufu imeshuhudia mamia ya watu waliokuja kuhuisha siku za Lailatul-Qadri kwa kufanya ibada mbalimbali, eneo hilo linamazingira mazuri kiroho na kiibada”.

Akaongeza kuwa “Ratiba za kiibata ni sehemu muhimu ya harakati za idara, zimekua zikifanywa kila mwaka na kupata mafanikio makubwa, mahudhurio yamekua yakiongezeka mwaka hadi mwaka na malengo yanafikiwa”.

Ratiba ya mwezi wa Ramadhani mwaka huu, imekuwa na vipengele vingi vya kiibada kwa lengo la kunufaika na baraka za mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: