Wanafunzi wa Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake wamekuwa washindi wa kwanza kwenye mashindano ya Qur’ani yaliyoandaliwa na wizara ya malezi.

Wanafunzi wa Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake chini ya ofisi ya Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, wamekuwa washindi wa kwanza kwenye mashindano ya Qur’ani yaliyoandaliwa na wizara ya malezi.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi amesema “Wanafunzi wa Maahadi kutoka tawi la Waasit wamekuwa washindi wa kwanza kwenye mashindano ya kuhifadhi Qur’ani yaliyofanywa na wizara ya malezi kwenye mikoa yote ya Iraq kwa wanafunzi wa ngazi zote”.

Akaongeza kuwa “Mwanafunzi (Ghadiir Abdul-Hussein Abdu) amekuwa mshindi wa kwanza katika ngazi ya wanafunzi wa sekondari (upili), huku (Ruqayya Abdullah Madh-haru) akiwa mshindi wa pili katika ngazi hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: