Maelfu ya mazuwaru wanahuisha usiku wa Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani katika mji wa Karbala.

Ataba mbili tukufu zimeshuhudia makundi makubwa ya mazuwaru kutoka Maelfu ya mazuwaru wamehuisha usiku wa Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mji wa Karbala.

ndani na nje ya Iraq, waliokuja kufanya ziara na kusoma dua mbele ya malalo mbili takatifu jioni ya siku ya Alkhamisi.

Mazuwaru katika siku hizi tukufu huswali kwa wingi, husoma dua, hutembelea malalo ya Ahlulbait (a.s) na kusoma Qur’ani.

Atabatu Abbasiyya tukufu imejiandaa vilivyo katika kupokea mazuwaru wanaokuja kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kuwapa huduma mbalimbali ikiwepo futari, kuandaa sehemu maalum za kuswalia na kusoma dua ndani ya haram tukufu na maeneo yanayozunguka Ataba takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: