Kitengo cha habari na utamaduni kimefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani nchini Senegal.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani kwa mayatima nchini Senegal.

Kikao kimeratibiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya kupitia ratiba ya mwezi wa Ramadhani.

Muwakilishi wa Markazi nchini Senegal Shekhe Mustwafa amesema “Ratiba ya mwezi wa Ramadhani bado inaendelea hapa Senegal, inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele vyake ni vikao vya usomaji wa Qur’ani katika kituo cha kulelea Watoto yatima”.

Akaongeza kuwa “Ratiba hiyo inalenga kujenga uhusiano baina ya mayatima na Qur’ani na kuwafundisha hukumu za usomaji na uwelewa wa kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: