Ofisi ya kiongozi mkuu tawi la wanawake imehitimisha hafla za usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani kwa wanawake.

Ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha hafla za usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani katika Atabatu Alawiyya takatifu.

Kiongozi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake bibi Taghridi Tamimi amesema “Ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria tawi la wanawake, imehitimisha vikao vya usomaji wa Qur’ani kwa wanawake ndani ya mwezi wa Ramadhani katika kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s), kwa uhudhuriaji wa washiriki (250), hafla ya mwisho imefanywa ndani ya haram ya Atabatu Alawiyya sambamba na ziara ya malalo ya kiongozi wa waumini (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Lengo la ratiba ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambayo imehitimishwa ndani ya haram ya kiongozi wa waumini, ni kuwaunganisha mazuwaru na kiongozi wa waumini (a.s) katika siku kumi za mwisho wa Mweni wa Ramadhani”.

Akaendelea kusema “Ratiba ya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani inasaidia kujenga uwelewa wa Qur’ani na utamaduni kwa wanawake”, akasema kuwa “Atabatu Alawiyya iliandaa kila kitu kinachohitajika katika hafla ya ufungaji wa ratiba hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: